
 BONGO CAMPING TUKUYUBONGO CAMPING
1.MRADI WA MAENDELEO NA MALENGO YAKE
Maelezo kwa ufupi
Baada ya kuona ya kwamba watalii wamezidi na kuona kuna uwezekano wa utalii mkoani Mbeya, na hasa wilaya ya Rungwe kuna uwezekano wa kuweka camping site, mashirika hayo mawilli yameamua kuuandaa mradi wa maendelo wa miaka miwili uitwao Bongo Camping. Makadilio ya kuanzisha mradi huo ni tarehe 1/4/2007.
Lengo kuu la mradi: Mradi huo wa miaka miwili utasababisha chama cha KUMBE kiwe na nguzo ya kujitegemea kwa kuendeleza utalii Mkoani Mbeya ili chama kifanikiwe na malengo yake ya kimaendeleo.
Kufuatana na matarajio ya bajeti ofisi ya Bongo Camping itafunguliwa kijiji cha Kibisi. Vilevile washiriki wanatafuta ofisi mjini Tukuyu ili kuuboresha uratibu wa IT na kuwa na mapokezi ya watalii wanaopita mjini.
Wafadhili wa mradi wa Bongo Camping ni wadenmark binafsi. Wafadhili hao wako tayari kutoa shilingi milioni arobaini na tatu ilimradi masharti yao yafuatayo yakamilishwe: Kutakuwa na mfanyakazi mmoja kutoka Chama cha BDT ambaye atausimamia mradi akiwa anasaidiana na msimamizi wa KUMBE na wanachama kwa ujumla. Pia washiriki wote wamekubadiliana mfanyakazi huyo lazima awe na ujuzi wa kompyuta, UKIMWI, kiswahili na kiingereza ili kusaidiana zaidi. Mfanyakazi huyo wa nje pia awe anayeyafahamu mazingira ya mkoa wa Mbeya.
Sharti lingine ni wafanyakazi wa KUMBE na BDT wataukagua mradi kila mwezi wakiwa wanashauriana na mkaguzi wa uchumi kutoka BDT.
Vitakavyokuwepo katika mradi ni kama vifuatavyo: kujenga nyumba ya utalii na elimu, kujenga nyumba ya viongozi, kusukuma utalii, kuhudumia malazi, kuwatembeza watalii, na kutoa huduma za IT. Pia tutaitafuta nafasi ya kufungua ofisi nyingine mjini Tukuyu.
Maelezo kwa ndani zaidi. Sehemu kuu nne za Bongo Camping kwa ajili ya malengo ya muda mrefu katika maendeleo ya Mkoa wa Mbeya.
1) Utalii
Idadi ya watalii
Kufuata matarajio ya bajeti ya Bongo Camping watafika watalii 50 mwaka wa kwanza. Baada ya kukamilisha ujenzi idadi ya watalii itaongezeka iwe 150 mwaka wa pili. Hayo ni makadirio yetu ya chini ambayo yanafuatana na hali ilivyo kaika eneo tulilonalo (rejea bajeti). Mwaka wa tatu baada ya kuukamilisha mradi wa miaka miwili makadirio yatakuwa juu takriban asilimia 25 tukifanikiwa na shughuli zifuatazo:
-Tutafanya kazi ya kutangaza camping na eneo kwa ujumla ili watalii wavutiwi zaidi.
-Tayari tumeianzisha tovuti ya mtandao (mwezi wa 6 mwaka 2006), tovuti hiyo tutaiboresha siku hadi siku. Ili kusukuma matangazo ya mkoa wa Mbeya tumeshirikiana na www.uwazi.com
- Tutawasiliana na watanzania wenzetu wenye tovuti za mtandao.
- Tunalenga kutangaza jina <personname productid="la Mbeya" w:st="on">la Mbeya</personname> na jina <personname productid="la Bongo Camping" w:st="on"><personname productid="la Bongo" w:st="on">la Bongo</personname> Camping</personname> katika kitabu cha Lonely Planet, vitabu vya utalii vya kiafrika na vitabu vingine vya usafiri katika bara <personname productid="la Afrika." w:st="on">la Afrika.</personname>
- Tunalenga kushirikiana na vyombo vya utalii nchini Tanzania na katika nchi za nje.
- Tutatengeneza vipeperushi na kuvisambaza ambapo watalii watakuwepo, kwa mfano mjini Mbeya, treni ya Tazara, Boda ya Malawi na Boda ya Zambia.
- Tunalenga kusaidiana na wanachama wa BDT kutangaza nchini Denmark, ili tuvikaribishe vikundi vya taasisi za jamiii waje kutembelea mkoani Mbeya.
- Tutatoa huduma ya kuwatembeza watalii hadi vivutio vizuri vifuatavyo katika mkoa wa Mbeya:
Matema Beach (muda wa siku 1 hadi 3),
Ngozi Crater Lake (muda wa siku 1),
Mlima Rungwe (muda wa siku 1 hadi 2),
Daraja <personname productid="la Mungu" w:st="on">la Mungu</personname> / Natural Bridge (muda wa siku 1),
Maporomoko ya maji ya Kaporogwe (muda wa siku 1)
Maporomoko ya maji ya Marasusi (muda wa siku 1),
Masoko Crater Lake (muda wa siku 1)
Historia mjini Tukuyu (muda wa siku 1)
(rejea www.bongocamping.com kwa picha na maandiko mengine mengi).
- Mwaka wa kwanza na wa pili tutawashirikisha waongozi wa utalii waliopo katika eneo la camping. Waongozi ambao tayari tumewasiliana nao ni wanachama wa KUMBE ambao wana ujuzi wa muda mrefu katika kuwatembeza watalii katika vivutio vilivyotajwa hapo juu.
- Wakati wa kuwashirikisha waongozi wa utalii pia tutayaangalia malengo ya usafi wa mazingira ambao ni suala la muhimu sana katika chama cha KUMBE.
2) Masuluhisho ya UKIMWI
UKIMWI na virusi vyake ni miongoni mwa magonjwa yanayotisha na yanayoathili uchumi wa Taifa pamoja na maeneo hayo ya Nyanda za juu Kusini hasa Mkoa wa Mbeya kama ilivyo sehemu nyinginezo Nchini.
Wafanyakazi wa Bongo Camping ikiwa pamoja na msimamizi aliyetumwa kutoka nchi ya Denmark wana ujuzi wa shughuli za kutafuta masuluhisho ya UKIMWI. Wakiwa wanasaidiana katika shughuli hizo washiriki wa Bongo Camping wanalenga kusaidia watu waishio katika hali ya hatari <personname productid="la UKIMWI" w:st="on">la UKIMWI</personname> kwa kuwaelekeza njia fasaha za kujikinga na ugonjwa huo pia namna bora ya matumizi sahihi ya njia kuu tatu za kuweza kuzifuata ili kuepukana na maambukizo ya ugonjwa huo.
Pia lengo la washiriki wa Bongo Camping ni kuwasaidia viongozi wa vikundi na mashirika mbalimbali ya eneo tulilonalo kwa njia ya kuwapa mbinu za kujadiliana suala <personname productid="la UKIMWI" w:st="on">la UKIMWI</personname> katika vikundi vyao.
Ili kufikia malengo hayo wafanyakazi wa Bongo Camping wataanza kutoa elimu ya UKIMWI kwa ajili ya wanachama wa KUMBE (rejea ratiba za elimu).
Pia ni msimamo wetu kujadiliana suala <personname productid="la UKIMWI" w:st="on">la UKIMWI</personname> kwa uwazi katika chama cha KUMBE ili wanachama na wafanyakazi wa Bongo Camping waweze kutoa mifano mizuri mbele ya jamii na mashirika mengine.
3) Kompyuta na IT
Kufuatana na matarajio ya bajeti ofisi ya Bongo Camping itafunguliwa kijiji cha Kibisi. Vilevile washiriki wanatafuta ofisi mjini Tukuyu ili kuuboresha uratibu wa IT na kuwa na mapokezi ya watalii wanaopita mjini.
Lengo letu la muda mrefu ni kuongoza katika maendeleo ya IT mkoani Mbeya. Siku hizi shughuli za IT hazina mafanikio sana ila tunatarajia kuziboresha zaidi na kuzikuuza. Tayari wataalamu wa IT kutoka chama cha Bongo Development Tourism wamewashirikisha wanachama wa KUMBE katika mpango wa www.uwazi.com ambao utakuwa mlango wa matangazo na mawasiliano katika mkoa wa Mbeya.
Njia ya kwanza kufanikiwa na lengo hilo ni kubadilishana ujuzi na akili na wanachama wa BDT ambao wamejitolea kuwasaidia wafanyakazi wa Bongo Camping hatua mbalimbali za kunendeleza IT na matangazo ya mtandao.
Njia ya pili kufanikiwa na lengo <personname productid="la IT" w:st="on">la IT</personname> ni kuwafundisha wanachama wa KUMBE waanze kujua jinsi ya kutumia kompyuta na mtandao (rejea ratiba ya elimu na maelezo ya nafasi za kazi).
Pia ujuzi wa kompyuta na IT utaweza kusaidia katika malengo yote ya utalii kwa njia ya mawasiliano na mahusiano mazuri kati ya wageni na wenyeji. Hayo yote yatawawezesha wanachama wa KUMBE wayakamilishe malengo yao ya kimaendeleo.
4) Lugha za kimataifa
Kiswahili kitakuwa lugha ya kikazi katika mradi wa Bongo Camping. Vilevile wanachama wameona umuhimu wa kujifunza lugha zingine za kimataifa hasa lugha ya kiingereza.
Faida ya kujifunza kiingereza wanachama wa KUMBE waweze kujitegemea kilugha katika shughuli zao mbalimbali.
Mtu wa nje kutoka Bongo Development Tourism aliyechaguliwa kuwa msimamizi wa mradi wa miaka miwili amejitolea kuchukua nafasi hiyo ya kufundisha kiingereza akiwa anasaidiana na watanzania wengine wenye
ujuzi huo.
Washiriki wamepanga shughuli itakayotuwezesha kufanikiwa na nia hiyo ya lugha. Wanachama wa KUMBE watafundishwa kiingereza katika uwanja wa camping (rejea ratiba ya elimu na maelezo ya nafasi za kazi).
Majirani wa camping katika kijiji cha Kibisi
Washiriki wa mradi wa maendeleo wa Bongo Camping wamependelea uhusiano mzuri kati ya majirani na wafanyakazi wa Bongo Camping.
Kwa hiyo viongozi wa kijiji cha Kibisi watakaribishwa kwenye mkutano kabla ya mradi haujafunguliwa.
Nia ya mawasiliano kati ya wafanyakazi wa Bongo Camping na wanakijiji wa Kibisi ni kuwa na ujirani mwema na kubadilishana mawazo pale panapotakiwa.
Pia nia ya mawasiliano hayo ni kuwakaribisha wanakijiji wa Kibisi wajiunge katika chama cha KUMBE ili baadaye waweze kusaidia katika kazi za maendeleo na katika miradi mingine ijayo.
Zaidi ya hayo wanachama wa KUMBE watapenda kuwatia moyo wanakijiji katika changamoto ya UKIMWI.
Matarajio ya baadaye ya Bongo Camping
Wanachama wa KUMBE na washiriki wa Bongo Camping wameweka malengo ya baadaye. Baada ya kufanikiwa na kazi za mradi huo wa miaka miwili wanalenga kuzifungua camping zingine katika mkoa wa Mbeya.
Katika mkoa wa Mbeya maendeleo ya utalii na ya elimu yako nyuma kwa ujumla. Wanachama wa KUMBE wameona kuna sehemu zingine mkoani zinazofaa kwa kufunguliwa camping sites – kwa mfano kwenye boda ya Malawi na kwenye boda ya Zambia pia.
Katika mradi wa Bongo Camping washiriki wataangalia matarajio hayo ya baadaye wakati wanatafuta njia za kujitegemea na kufanya mapato yao ya maendeleo yaongezeke.
Matarajio hayo ya baadaye tumeyaonyesha hapo chini kwa kuchora nembo za camping. Fremu ya nembo haitabadilika lakini picha zilizopo ndani yake zitakuwa zinaonyesha sanaa tofauti. Ina maana mabadiliko na maongezeko ya Bongo Camping yataonyeshwa kwa njia ya kutangaza nembo walizochora wasanii wanaosaidia katika miradi ya KUMBE.
Kwa njia ya kuchora nembo hizo tunataka kuwahakikishia watu kwa ujumla na hasa wanaotupa msaada wa maendeleo ya kwamba washiriki wa Bongo Camping wana nia nzuri ya kuleta maendeleo.
Mifano ya nembo: (pia rejea ”daftari ya nembo” katika kurasa ifuatayo).
Bongo Camping Bongo Camping Bongo Camping
Tukuyu (2007-) Tunduma (2011-) Kyela (2013-)
<shapetype coordsize="21600,21600" o:spt="75" o:preferrelative="t" path="m@4@5l@4@11@9@11@9@5xe" filled="f" stroked="f" id="_x0000_t75"><stroke joinstyle="miter"></stroke><formulas><f eqn="if lineDrawn pixelLineWidth 0"></f><f eqn="sum @0 1 0"></f><f eqn="sum 0 0 @1"></f><f eqn="prod @2 1 2"></f><f eqn="prod @3 21600 pixelWidth"></f><f eqn="prod @3 21600 pixelHeight"></f><f eqn="sum @0 0 1"></f><f eqn="prod @6 1 2"></f><f eqn="prod @7 21600 pixelWidth"></f><f eqn="sum @8 21600 0"></f><f eqn="prod @7 21600 pixelHeight"></f><f eqn="sum @10 21600 0"></f></formulas><path o:extrusionok="f" gradientshapeok="t" o:connecttype="rect"></path><lock v:ext="edit" aspectratio="t"></lock></shapetype><shape type="#_x0000_t75" style="WIDTH: 92.25pt; HEIGHT: 100.5pt" id="_x0000_i1025"><imagedata src="file:///C:\DOCUME~1\KASPER~1\LOKALE~1\Temp\msohtml1\01\clip_image001.png"></imagedata></shape> <shape type="#_x0000_t75" style="WIDTH: 96pt; HEIGHT: 100.5pt" id="_x0000_i1026"><imagedata src="file:///C:\DOCUME~1\KASPER~1\LOKALE~1\Temp\msohtml1\01\clip_image003.jpg" o:title="logoshlom7"></imagedata></shape> <shape type="#_x0000_t75" style="WIDTH: 94.5pt; HEIGHT: 99.75pt" id="_x0000_i1027"> <imagedata src="file:///C:\DOCUME~1\KASPER~1\LOKALE~1\Temp\msohtml1\01\clip_image005.jpg" o:title="logoshlom1"></imagedata></shape>
DAFTARI YA NEMBO
Daftari hiyo itaonyesha mifano ya nembo za Bongo Camping zenye picha walizochora wasanii wanaotusaidia chama cha KUMBE na cha Bongo Development Tourism.
Nembo ziko tofauti ila picha zote, ziwe zilizotengenezwa au zitakazotengenezwa, zitaonyesha utamaduni na desturi za kikabila na urafiki uliopo kati ya wageni na wenyeji.
Mradi wa Bongo Camping utakapofunguliwa washiriki wataanza kuziuza nembo kwa watalii na kwa mtu yeyote anayetaka kunufaika. Faida ya nembo zitatumika kwa ajili ya mradi wa maendeleo pamoja na kumpa msanii aliyechora nembo kiasi chake. Hivyo washiriki wa Bongo Camping wanaweza kutangaza mradi wa Bongo Camping pamoja na kuwasaidia vijana wenye vipaji vya kisanii.
Joseph John (Msanii, Songea) Kasper Gram-Hansen
<shape type="#_x0000_t75" style="WIDTH: 104.25pt; HEIGHT: 101.25pt" id="_x0000_i1028"><imagedata src="file:///C:\DOCUME~1\KASPER~1\LOKALE~1\Temp\msohtml1\01\clip_image007.png"></imagedata></shape> <shape type="#_x0000_t75" style="WIDTH: 92.25pt; HEIGHT: 100.5pt" id="_x0000_i1029"> <imagedata src="file:///C:\DOCUME~1\KASPER~1\LOKALE~1\Temp\msohtml1\01\clip_image001.png"></imagedata></shape>
Shlomik Avshalom (Msanii, Denmark)
<shape type="#_x0000_t75" style="WIDTH: 97.5pt; HEIGHT: 102pt" id="_x0000_i1030"> <imagedata src="file:///C:\DOCUME~1\KASPER~1\LOKALE~1\Temp\msohtml1\01\clip_image010.jpg" o:title="logoshlom2"></imagedata></shape> <shape type="#_x0000_t75" style="WIDTH: 96pt; HEIGHT: 101.25pt" id="_x0000_i1031"><imagedata src="file:///C:\DOCUME~1\KASPER~1\LOKALE~1\Temp\msohtml1\01\clip_image012.jpg" o:title="logoshlom3"></imagedata></shape> <shape type="#_x0000_t75" style="WIDTH: 96pt; HEIGHT: 102pt" id="_x0000_i1032"> <imagedata src="file:///C:\DOCUME~1\KASPER~1\LOKALE~1\Temp\msohtml1\01\clip_image014.jpg" o:title="logoshlom5"></imagedata></shape> <shape type="#_x0000_t75" style="WIDTH: 95.25pt; HEIGHT: 102pt" id="_x0000_i1033"> <imagedata src="file:///C:\DOCUME~1\KASPER~1\LOKALE~1\Temp\msohtml1\01\clip_image016.jpg" o:title="logoshlom6"></imagedata></shape>

|